Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuomba Mufti wa Zanzibar, Salehe Kaab, kukutana na Maalim Seif Shariff Hamad ili kumfikishia ‘ujumbe wake’. Taarifa zilizotufikia jioni ya leo zinaeleza kuwa Mufti Kaab tayari ameomba miadi ya kukutana na Maalim Seif sikiu ya Jumapili, Novemba 8, 2020 Chanzo cha IMEVUJA kimeeleza kwamba Mufti Kaab amebeba ujumbe wa Rais Dkt. Mwinyi unaoomba ...
Vyanzo vyetu vya uhakika vinadokeza kuwa huduma ya Mawasiliano ya Mitandao ya kijamii zitaanza kurejea kuanzia kesho Novemba 7. Mojawapo ya vyanzo vyetu kimetudokeza kuwa watoa huduma (ISP) wameshaanza kupewa maelekezo kuanzia leo warejeshe huduma hiyo ili wananchi wapate kuwasiliana bila vikwazo kama ilivyokuwa hadi tunaandika taarifa hii. Mitandao mingi ya kijamii ilizuiliwa (blocked) kuanzia Oktoba 27, 2020 ikiwa ni ...
Viongozi wa CHADEMA, Freeman A. Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Taifa na aliyekuwa Mbunge na mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless J. Lema walihamishiwa kituo cha Mlandizi mkoani Pwani juzi. Haijafahamika mara moja lengo la kuwatenganisha na wenzao na sababu hasa za kupelekwa Pwani ingawa chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi kinabainisha kuwa lengo lilikuwa ni ...
Polisi wamerandaranda sehemu alipo Lissu ili wamkamate upya. Taarifa kutoka chanzo cha uhakika zinadai makachero na Polisi wametanda kila sehemu wakisubiri atoke tu na kumtia mbaroni baada ya kubaini kuwa jana walikosea kumkamata eneo ambalo kwa mujibu wa Sheria ya Kimataifa ni makosa. Lissu akikamatwa, inasemekana atafunguliwa mashtaka ya uhaini (si ugaidi) na mkakati ni kuhakikisha anabaki kizuizini kwa muda ...
Vikosi vya Usalama visiwani Zanzibar sasa hivi vipo njiani kumrudisha Maalim Seif nyumbani kwake akiwa chini ya ulinzi mkali. Sharti ni asitoke ndani, abaki nyumbani kwake. Wakati huohuo, vikosi vya usalama vinaendelea kutembeza vipigo kwa wananchi maeneo ya Mtendani visiwani Zanzibar kwa wafuasi wa upinzani ambao wanataka kupiga kura leo badala ya kesho. ...
Katika Jimbo la Pangawe, Shehia ya Kijitoupele, Unguja, vijana wa CCM wameonekana wakisombwa na magari ya vyombo vya usalama kwa ajili ya kupiga kura za awali usiku huu. Vijana takribani 15 wameingia katika kituo cha kupigia kura cha Tanwiri, wakiwa wamebeba maboksi ambayo yanaonekana kuwa na karatasi za kura ndani yake. Magari ya Polisi ndiyo yamewashusha vijana hao na kuwasubiri ...
Vyombo vya usalama Zanzibar, usiku huu vimepanga kumzuia Maalim Seif Shariff Hamad asitoke nyumbani kwake, Chukwani, Zanzibar. Maalim Seif, ambaye ni mgombea urais visiwani humo kupitia ACT – Wazalendo, katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar aliwaamuru wanachama na wafuasi wake kwenda kupiga kura kesho, Oktoba 27, siku ambayo ni maalum kwa baadhi ya ...
Ulinzi, upekuzi, kuhojiwa kumeimarishwa zaidi katika bandari na uwanja wa ndege wa Zanzibar, ikiwa ni siku mbili zikisalia kufika Oktoba 27, ili kuanza mchakato wa kupiga kura visiwani humo. Kura za awali zitapigwa keshokutwa, Oktoba 27, 2020 kwa watumishi wa Idara za Usalama, Majeshi na Watumishi wa Tume ya Uchaguzi. Hii ni ili kutoa nafasi kwa watendaji hao kushiriki kikamilifu ...
Mgombea urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad, leo anatarajiwa kutoa amri kwa wanachama na mashabiki wake kwenda vituo vya kupigia kura Oktoba 27, ili kuzuia kile anachoita “wizi wa kura na mbinu chafu kuvuruga uchaguzi.” Taarifa tulizopata asubuhi ya leo zinaonyesha kuwa Maalim Seif katika mkutano wake unaofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar, atawaamuru wafuasi wake kufanya hivyo ...
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Chama Cha Mapinduzi (CCM) na taasisi nyeti za serikali wanadaiwa kupanga kuhakikisha kura 40,000 zinapatikana siku moja kabla ya tarehe rasmi ya kupiga kura, Oktoba 28, 2020. Zanzibar imepanga kwa watumishi wa majeshi, idara za usalama na watumishi wa ZEC, kupiga kura Oktoba 27 ili kuwapa nafasi kutekeleza majukumu yao siku rasmi ya uchaguzi. Uchunguzi ...