Katika Jimbo la Pangawe, Shehia ya Kijitoupele, Unguja,  vijana wa CCM wameonekana wakisombwa na magari ya vyombo vya usalama kwa ajili ya kupiga kura za awali usiku huu. Vijana takribani 15 wameingia katika kituo cha kupigia kura cha Tanwiri, wakiwa wamebeba maboksi ambayo yanaonekana kuwa na karatasi za kura ndani yake. Magari ya Polisi ndiyo yamewashusha vijana hao na kuwasubiri ...

Vyombo vya usalama Zanzibar, usiku huu vimepanga kumzuia Maalim Seif Shariff Hamad asitoke nyumbani kwake, Chukwani, Zanzibar. Maalim Seif, ambaye ni mgombea urais visiwani humo kupitia ACT – Wazalendo, katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar aliwaamuru wanachama na wafuasi wake kwenda kupiga kura kesho, Oktoba 27, siku ambayo ni maalum kwa baadhi ya ...

Ulinzi, upekuzi, kuhojiwa kumeimarishwa zaidi katika bandari na uwanja wa ndege wa Zanzibar, ikiwa ni siku mbili  zikisalia kufika Oktoba 27, ili kuanza mchakato wa kupiga kura visiwani humo. Kura za awali zitapigwa keshokutwa, Oktoba 27, 2020 kwa watumishi wa Idara za Usalama, Majeshi na Watumishi wa Tume ya Uchaguzi. Hii ni ili kutoa nafasi kwa watendaji hao kushiriki kikamilifu ...

Mgombea urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo,  Maalim Seif Shariff Hamad, leo anatarajiwa kutoa amri kwa wanachama na mashabiki wake kwenda vituo vya kupigia kura Oktoba 27, ili kuzuia kile anachoita “wizi wa kura na mbinu chafu kuvuruga uchaguzi.” Taarifa tulizopata asubuhi ya leo zinaonyesha kuwa Maalim Seif katika mkutano wake unaofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar, atawaamuru wafuasi wake kufanya hivyo ...

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Chama Cha Mapinduzi (CCM) na taasisi nyeti za serikali wanadaiwa kupanga kuhakikisha kura 40,000 zinapatikana siku moja kabla ya tarehe rasmi ya kupiga kura, Oktoba 28, 2020. Zanzibar imepanga kwa watumishi wa majeshi, idara za usalama na watumishi wa ZEC, kupiga kura Oktoba 27 ili kuwapa nafasi kutekeleza majukumu yao siku rasmi ya uchaguzi.  Uchunguzi ...

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameweka kambi Zanzibar ili kuongeza nguvu katika kampeni za ushindi kwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Mzee Mwinyi, ambaye ni baba mzazi wa mgombea urais Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, amepewa makazi jirani na eneo la kupanga mikakati ya ushindi kwa mgombea huyo, Fumba. Timu binafsi ...

Taarifa tulizo nazo zinaonyesha Bwana Mkubwa anakulia timing tu, kuna mtu anaandaliwa kuishika nafasi yako wakati wowote baada ya Uchaguzi. Huyu ni naibu wako, Rodrick Mpogolo ambaye kina Polepole na Msigwa wanapambana kila uchao kuhakikisha anakuwa SG wa CCM na wewe ukachinjiwe baharini. Kimsingi, Polepole pia anaitamani nafasi yako. Huenda hujasoma alama za nyakati, sisi tunakudokeza mapema. Hiki ndo chanzo ...

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Josephat Gwajima amethibitika kugawa Sh. 20,000,000 kwa kila kata. Uchunguzi wetu umebaini kwamba mgombea huyo amekuwa akigawa kiasi hicho cha fedha kila anakopita kufanya kampeni. Jana katika Kata ya Msasani Kisiwani, Kinondoni, Gwajima akiwa katika kampeni alikutana na viongozi wa vikundi vya vijana vya ...

Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), imepunguza kiasi cha malipo ya wasimamizi wakuu wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. NEC imepunguza zaidi ya Sh. 100,000 mwaka huu, ikilinganishwa na uchaguzi uliopita, 2015. Taarifa zilizotufikia zinaonyesha kuwa mwaka huu, wasimamizi wakuu wa vituo watalipwa TSh. 105,000.  Katika uchaguzi uliopita walilipwa TSh. 210,00. Jumla ya wasimamizi wakuu ...

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, jana amewaeleza baadhi ya viongozi waandamizi na makada wa chama hicho kuwa wastahimilivu na waache kulalamika kuhusu fedha za kujikimu wakati wa kampeni. Kumekuwepo na manung’uniko kwa makada wa chama hicho ambao wanazunguka maeneo mbalimbali kuomba kura kwa wagombea wa CCM, kuanzia Rais, Wabunge na Madiwani. Dk. Bashiru anaelezwa kusema ...