PrecisionAir, Tanzania’s private commercial airline, has asked its staff, including pilots, to choose; either stay or leave.  In a June 27 internal memo, the airline’s management told staff who choose to leave to table a resignation letter and those opting to stay, write a commitment letter accepting salary cut.  The cut is said to stand down to a quarter of ...

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, wachapaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, imewataka waandishi wake wengi kuacha kazi au kubaki kuwa wachangiaji (correspondents). Wachangiaji katika Vyombo vya Habari hapa nchini hulipwa kwa habari (story) zinazochapishwa, wakati mwandishi hulipwa mshahara kwa mwezi. Hatua hii inatajwa kuwa ni njia ya kupunguza matumizi kutokana na kukumbwa na mdororo wa uchumi na ...

Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2020 wa kupata rais, wabunge na madiwani, utalazimika kutumia kiasi cha fedha kutoka Akiba ya Fedha za Kigeni (GOR). ​Hatua hii inatokana na Serikali kukwama kupata fedha za kutosha kugharamia uchaguzi huo kutoka kwa nchi wahisani kama ilivyozoeleka kwa miaka mingi. Sehemu kubwa ya fedha za Uchaguzi husimamiwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) na kwa ...

Pamoja na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais John Magufuli na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally kuonya viongozi wa chama ambao ni wasimamizi kutokuwa na wagombea wao mifukoni, hali imekuwa tofauti majimbo matatu ya mkoa wa Kilimanjaro. Haya ndo tuliyobaini kwa ufupi na uongozi wa CCM Taifa unaweza kutumia vyanzo vyake kubaini undani wa uchunguzi wetu: Jimbo ...

Ofisi ya mawakili wa kimataifa, Amsterdam and Partners inayoshika mikoba ya kumwakilisha Tundu Lissu kisheria, imesema inajiandaa kutangaza matokeo ya uchunguzi juu ya kushambuliwa kwa mteja wake. Taarifa zinaeleza kuwa mawakili hao wanajiandaa kutangaza matokeo ya uchunguzi wao muda wowote kuanzia sasa baada ya kile kinachoelezwa “Serikali kushindwa majukumu yake.” Inaelezwa kuwa mawakili hao mara baada ya kupewa kandarasi ya kumsimamia ...

YAMEIBUKA madai mazito ya uwepo wa matukio ya rushwa kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya ubunge jimbo la Arusha Mjini. Mbinu alizotumia Makonda huko Kigamboni zinafanana. Aidha msimamizi wa Uchaguzi huo adaiwa kuonyesha upendeleo wa wazi kwa baadhi ya wagombea kwa kuzuia mmoja wa wagombea asiulizwe maswali licha ...

Mkakati wa timu ya Makonda kuhakikisha zinapatikana kura nyingi za maoni kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu Jimbo la Kigamboni uligubikwa kwa rushwa, imebainika. Rushwa hiyo iliyotembezwa waziwazi kwa wajumbe wa mkutano huo uliomalizika leo, imedhihiri baada ya wapambe wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuanza kuwatukana na kuwatisha baadhi ya wajumbe hao. Waliokula pesa ...

Waandishi wa Habari na Watumishi wa Vyombo vya Habari nchini waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wamegeuka ombaomba. Waandishi na watumishi hao wanaofikia 31; huku 29 wakiomba kuteuliwa na chama tawala, CCM na wawili kupitia CHADEMA, wamekuwa wakihaha kusaka fedha ili kufanikisha azma zao. Uchunguzi wetu umebaini kuwa waandishi waliothibitika kuhangaika zaidi kuomba msaada wa kifedha ni wale waliotia nia ...

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa na Jeshi la Polisi siku nane zilizopita (Julai 9, 2020) yuko Kituo cha Polisi Magomeni jijini Dar es Salaam. Vyanzo vyetu vya uhakika vimebainisha kuwa Ponda alihamishiwa kituoni hapo juzi usiku akitolewa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar. Hata hivyo, uwepo wa Sheikh huyo katika kituo hicho umekuwa ...

Uamuzi wa Paul Makonda kuacha ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwenda kuomba ridhaa ya chama chake kugombea ubunge, unachambuliwa kwa namna mbili kuu: Amejaa kiburi au kuwa na uthubutu usiomithilika. Tayari Makonda amechukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Kigamboni, Dar es Salaam na ameirejesha leo. Kumekuwepo na hisia tofauti juu ya uamuzi huo wa Makonda, wachambuzi ...