YAMEIBUKA madai mazito ya uwepo wa matukio ya rushwa kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya ubunge jimbo la Arusha Mjini. Mbinu alizotumia Makonda huko Kigamboni zinafanana. Aidha msimamizi wa Uchaguzi huo adaiwa kuonyesha upendeleo wa wazi kwa baadhi ya wagombea kwa kuzuia mmoja wa wagombea asiulizwe maswali licha ...

Mkakati wa timu ya Makonda kuhakikisha zinapatikana kura nyingi za maoni kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu Jimbo la Kigamboni uligubikwa kwa rushwa, imebainika. Rushwa hiyo iliyotembezwa waziwazi kwa wajumbe wa mkutano huo uliomalizika leo, imedhihiri baada ya wapambe wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuanza kuwatukana na kuwatisha baadhi ya wajumbe hao. Waliokula pesa ...

Waandishi wa Habari na Watumishi wa Vyombo vya Habari nchini waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wamegeuka ombaomba. Waandishi na watumishi hao wanaofikia 31; huku 29 wakiomba kuteuliwa na chama tawala, CCM na wawili kupitia CHADEMA, wamekuwa wakihaha kusaka fedha ili kufanikisha azma zao. Uchunguzi wetu umebaini kuwa waandishi waliothibitika kuhangaika zaidi kuomba msaada wa kifedha ni wale waliotia nia ...

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa na Jeshi la Polisi siku nane zilizopita (Julai 9, 2020) yuko Kituo cha Polisi Magomeni jijini Dar es Salaam. Vyanzo vyetu vya uhakika vimebainisha kuwa Ponda alihamishiwa kituoni hapo juzi usiku akitolewa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar. Hata hivyo, uwepo wa Sheikh huyo katika kituo hicho umekuwa ...

Uamuzi wa Paul Makonda kuacha ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwenda kuomba ridhaa ya chama chake kugombea ubunge, unachambuliwa kwa namna mbili kuu: Amejaa kiburi au kuwa na uthubutu usiomithilika. Tayari Makonda amechukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Kigamboni, Dar es Salaam na ameirejesha leo. Kumekuwepo na hisia tofauti juu ya uamuzi huo wa Makonda, wachambuzi ...

Tanzania bado inaendelea kuficha taarifa za maambukizi ya virusi vya Corona, hata hivyo vifo vinavyotokana na ugonjwa huo vinaiumbua. Taarifa za kitabibu na maabara tulizo nazo zinaonyesha ugonjwa huo bado upo na usiku wa kuamkia jana “changamoto ya upumuaji” imeuchukua uhai wa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Salvatory Bongole. Uchunguzi wetu katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora, Kitete umebaini ...

Kampuni iliyofichwa na TAKUKURU baada ya kumkamatisha rushwa mhariri wa gazeti la Kiswahili la Serikali, HabariLeo, Oscar Mbuza, imebainika kuwa ni Kamal Steels Limited iliyo na ofisi zake Kitalu namba 188/2, Barabara ya Mwakalinga eneo la viwanda Chang’ombe – Temeke, Dar es Salaam. Katika taarifa yake kwa umma kuhusu kukamatwa kwa Mhariri huyo iliyotolewa Juni 30, 2020, TAKUKURU ilificha jina ...

Shamrashamra na makeke ya kisiasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar yameshindwa kuonekana katika vijiwe maarufu vya mashabiki wa chama hicho – maskani, baada ya Dkt. Hussein Mwinyi kuteuliwa kuwania urais wa visiwa hivyo. Vijiwe maarufu kikiwemo Kisonge, maeneo ya Michenzani, Zanzibar, hakuonekani kuwa na uhai tangu kutangazwa kwa Dkt. Mwinyi jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Katika mbao maarufu za ...

Serikali imeamua kula matapishi yake baada ya leo kubadili msimamo wake kumkamata Tundu Lissu atakaporejea nchini. Katika mahakama ya Kisutu, Serikali kupitia wakili wake mwandamizi, Simon Wankyo imeieleza mahakama itupilie mbali maombi ya wadhamini wake, Robert Katula na Ibrahim Ahmed wanaotaka kujiondoa udhamini kwa Lissu katika kesi ya jinai inayomkabili. Serikali kupitia hati kinzani dhidi ya maombi ya wadhamini hao, ...

Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula ameomba kupumzika kazi hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu. Barua aliyoandika Juni 22, 2020 kwenda kwa Mwenyekiti wake, John Pombe Magufuli, inaeleza kuwa anaomba kupumzika kutokana na kuwa na umri mkubwa na changamoto  za afya. Hivi sasa Mangula ana miaka 79. Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa Mangula aliomba kupumzika ...