Julius Kalanga, aliyekuwa Mbunge wa Monduli atiwa nguvuni

Aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga anashikiliwa na kikosi kazi cha Serikali kutoka Makao Makuu Dar, kinachohusika na kukusanya madeni.

Taarifa za uhakika zinasema Kalanga amekamatwa leo majira ya jioni nje ya ofisi za NMB na askari wa Takukuru na baadaye kupelekwa ofisi za TAKUKURU mkoa.

Akiwa njiani inadaiwa alikuwa akilalamika kwamba Mdhamini wake wa Mkopo huo Ndugu Kadogoo amemkimbia na hapokei simu zake tena.

“Juzi alikamatwa na kudhaminiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli, Isack Matasia aka Kadogo. Tumemsaka Kadogo hapatikani, lakini tumemtia nguvuni, leo tupo naye,” kimesema chanzo chetu.

Kalanga anadaiwa kukopa matrekta kutoka NDC na amekimbia kulipa deni na kuzima simu.

Maofisa wa Serikali waliopiga simu kupata taarifa, inadaiwa wamechimbwa mkwara mzito na Ofisi ya Mkuu Mkoa, Idd Kimantha.