Ofisa Mtendaji Mkuu wa Clouds Media Group (CMG), Joseph Kusaga anatuhumiwa kufuja fedha za kampuni, matumizi mabaya ya uongozi na dhuluma kwa wanahisa wengine, zikiwemo za marehemu baba yake.
Taarifa zilizotufikia zinaonyesha kuwa Joseph, maarufu kwa jina la Joe, amekuwa akitumia fedha zinazopatikana kupitia Clouds FM, kuanzisha biashara binafsi, kukwapua mali, hasa nyumba na mashamba ambayo yalinunuliwa kwa fedha za Clouds Entertainment Company Limited. Mali hizo za mabilioni, zinatajwa kuwepo Arusha, Dar es Salaam na maeneo ya Mkoa wa Pwani, Kijiji cha Fukayosi.
Joe, pia anatajwa kutumia rasilimali za kampuni mama kuanzisha radio na biashara Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu. Pia biashara ya kuuza karanga, aliyokuwa akisimamia mwanamuziki, Diamond Platinums, Wasafi FM, Spice FM na biashara nyingine, zinaelezwa kusajiliwa kwa kuonyesha zinamilikiwa na mkewe, Juahyna na watoto wake wawili.
Pia inaelezwa kuwa maisha familia yake Dubai, ambako alihamia mwaka 2012 yanagharimiwa na Clouds bila makubaliano ya wanahisa wengine na familia yake kwa ujumla. Watoto wake wanadaiwa kuwa wanasoma huko kwa gharama za kampuni.
Taarifa zinaonyesha kuwa watoto hao wanalipiwa Saudi ya shilingi milioni 400 kwa mwaka katika shule ya Kimataifa. Gharama hizo hubebwa na kampuni iliyoanzishwa kwa ushirikiano wa familia ya Kusaga.
Hadi mwaka 2016, Clouds inatajwa kukusanya zaidi ya Sh. bilioni 14 kwa kila mwaka.
TAARIFA ZILIZOVUJA:
Leave a Reply